Ruka hadi maudhui
AzamPesa
Pakua App

AzamPesa

Huduma za Benki

Huduma za Kibenki na AzamPesa.

Kijana mwenye miwani akiangalia simu yake mtaani
Kutoka benki

TSh 150,000

Imehamishwa ✓

Kuhusu Huduma

AzamPesa inakuwezesha kufanya huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi.

  • AzamPesa kwenda BenkiUnaweza kuhamisha pesa kutoka AzamPesa kwenda kwenye akaunti ya benki.
  • Benki kwenda AzamPesaUnaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yako ya benki kwenda AzamPesa.
  • Unganisha namba yakoMteja anatakiwa kuunganisha namba yake ya simu na akaunti yake ya benki kuweza kufanya huduma hizi.

Jinsi Inavyofanya Kazi

Au kwa USSD: piga *150*08#, chagua 6 Huduma za Benki, chagua 1 AzamPesa kwenda Benki AU 2 Benki kwenda AzamPesa, kisha chagua Benki na ufuate maelekezo.

  1. Hatua 1Fungua App ya AzamPesa
  2. Hatua 2Bofya Hamisha kwenda Benki
  3. Hatua 3Weka Akaunti Namba
  4. Hatua 4Weka Kiasi
  5. Hatua 5Hakiki taarifa zako, kisha Bofya Thibitisha Tuma
  6. Hatua 6Weka PIN yako ya AzamPesa, kisha Thibitisha

Baadhi ya benki washirika

AzamPesa

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

i. Wakala wa AzamPesa: Tembelea wakala wa AzamPesa aliye karibu nawe ili kuweka pesa kwenye akaunti yako. Wakala wanapatikana:

  • Katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania
  • Katika ofisi zote za Posta Tanzania
  • Katika maduka ya Azam (Maduka ya Ice-cream ya Azam, maduka ya AzamTV, na maduka ya bidhaa za chakula za Azam)

ii. Pokea Pesa:

a) Kupokea kutoka kwenye pochi ya AzamPesa:

  • Piga 15008#
  • Chagua 1, Tuma Pesa
  • Chagua 1, Tuma Pesa kwenda AzamPesa
  • Weka namba ya AzamPesa ya mpokeaji
  • Weka kiasi
  • Weka PIN

b) Kupokea kutoka mitandao mingine ya simu:

  • Piga menyu ya huduma ya kutuma pesa ya mtandao husika
  • Chagua “Tuma Pesa”
  • Chagua “Tuma Pesa kwenda Mitandao Mingine”
  • Chagua kutuma kwenda AzamPesa
  • Weka namba ya simu iliyosajiliwa na AzamPesa (anza na 1 badala ya 0)
  • Weka kiasi
  • Weka PIN

c) Kupokea kutoka Benki: Unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka benki yoyote kwenda AzamPesa:

  • Ingia kwenye menyu ya huduma za benki
  • Chagua “Tuma Pesa kwenda Pochi ya Simu” au “Wallet”
  • Chagua AzamPesa
  • Weka namba ya AzamPesa iliyosajiliwa (anza na 1 badala ya 0)
  • Weka kiasi
  • Weka PIN

Benki washirika ni pamoja na: CRDB, NMB, NBC, Amana, BOA, ABSA, BancABC, Access Bank, NCBA, DCB, Exim Bank, Finca, Maendeleo Bank, PBZ, Stanbic Bank, TCB, Bank of India, Bank of Baroda, Canara, China Dasheng, MuCoBa, Mwanga Hakika, Habib, na ICB.

Huduma za Kibenki na AzamPesa

Kwa maelezo zaidi tembelea tawi lolote la benki unayotumia lililo karibu nawe.