

Gusa Kadi ya Malipo
Gusa kadi ni kadi ya malipo ambayo inaunganishwa moja kwa moja na waleti ya AzamPesa. Kadi ya Gusa inakuwezesha kufanya miamala yote na huduma zote za AzamPesa.
Kuhusu Gusa kadi
Gusa ni kadi ya malipo ambayo imeunganishwa moja kwa moja na waleti ya Azampesa.
Kadi ya Gusa inakuwezesha kufanya miamala yote na huduma zote za Azampesa.
Ili kupata kadi ya Gusa unatakiwa usajiliwe na AzamPesa na ufike kwa wakala wa AzamPesa anaefanya usajili wa Gusa kununua kadi ya Gusa.
Faida za kutumia kadi ya Gusa
- Kukata tiketi za mpira zinazochezewa Tanzania ( NBC, CAF )
- Kufanya miamala yote ya AzamPesa kupitia wakala wa Gusa. Mfano:Kutuma Pesa AzamPesa kwenda AzamPesa, Kununua muda wa maongezi, Kununua LUKU na Kulipa bili zote.
ZINGATIA
- Kadi moja ya Gusa inapatikana kwa Tsh 2000/=
- Kadi moja haiwezi kununua tiketi zaidi ya moja
- Namba moja ya AzamPesa inapata kadi moja

Faida, Viwango na Mawakala wa Gusa
Faida za kutumia kadi ya Gusa
- Kukata tiketi za mpira zinazochezewa Tanzania ( NBC, CAF )
- Kufanya miamala yote ya AzamPesa kupitia wakala wa Gusa. kama :Kutuma Pesa
- Kununua muda wa maongezi, Kununua LUKU na Kulipa bili zote.
Kiwango cha mwisho cha kufanya miamala na kadi ya Gusa
Kiwango cha kutuma na kutoa pesa ni Tsh. 5,000,000
Wapi wanapatikana mawakala wa Gusa
Kadi za Gusa zinapatikana maeneo haya:
- Makao makuu ya Azampesa Masaki
- Migodi yote ya AzamTv (Daresalaam)
- Mawakala wa Azampesa kivukoni na maeneo tofauti
- Baadhi ya maafisa mauzo (Freelancers)
Jinsi ya kununua Tiketi kwa Kadi ya Gusa
Jinsi ya kukata tiketi kwa kadi ya Gusa bila foleni, kirahisi popote ulipo
- Fungua app ya AzamPesa
- Bofya Kata Tiketi.
- Bofya “Tiketi Mpya.”
- Chagua “Tiketi za Mpira wa Miguu.”
- Chagua jina la mechi.
- Chagua aina ya tiketi.
- Kisha chagua GUSA katika aina ya kadi.
- Weka namba ya kadi.
- Endelea kukamilisha malipo.

Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
1. Endapo mteja atapoteza kadi ya Gusa
Mteja anapaswa kupiga simu huduma kwa wateja kwa msaada na ataweza kununua kadi nyingine baada ya kadi ya kwanza kufungwa
Muda wa matumizi wa kadi ya Gusa kuisha ni miaka mingapi?
Kadi haiishi muda, matumizi yake ni endelevu mpaka pale itakapoharibika ama kupotea.
3. Je, naweza kufanya malipo mtandaoni kwa kadi hii?
Hapana, huwezi kufanya malipo mtandaoni kwa sasa kwa kutumia kadi ya Gusa
4. Wapi naweza kununua kadi ya Gusa?
Kadi za Gusa unaweza kuzipata kwa mawakala waliopo
1.Migodi ya Azam TV (Dar es salaam)
2.AzamPay Masaki
3.Baadhi ya watu wa mauzo (Freelancers) na mawala wa Azampesa

Tutumie Ujumbe Leo
(WhatsApp)
0677 099 918

Tembelea Ofisi zetu
Makao Makuu
Haile Selassie Rd, Plot 208
Dar es Salaam, Tanzania

Tupigie Bure
Jumatatu – Ijumaa (Saa 24)
0800 785 555

Yote yaliyomo kwenye tovuti hii ni mali ya AzamPesa. Haki zote zimehifadhiwa. Hakimiliki.
Copyright 2025, AzamPesa