AZAMPESA FAQ

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

1. AzamPesa ni nini?

AzamPesa ni huduma ya pesa kwa njia ya simu inayokuwezesha kufanya miamala kwa gharama nafuu. Kama, kutuma na kupokea pesa, kununua muda wa maongezi, kulipa kwa simu kwa mfanyabiashara, kulipa bili kama Luku na maji, kufanya malipo ya serikali, kufanya miamala ya kibenki na kulipia huduma za Azam kama tiketi za Boti, Vifurushi vya ving’amuzi vya AzamTv na zaidi.

2. Jinsi gani naweza kujisajili na AzamPesa?

Taarifa unazohitaji kusajili AzamPesa:
– Namba ya NIDA
– Namba ya Simu
Njia mbalimbali unazoweza kutumia kujisajili:
i. Kujisajili mwenyewe
– Pakua App ya AzamPesa kwenye Google Play Store au iOS App Store
– Bonyeza USJILI BINAFSI chini ya INGIA
– Jaza namba yako ya simu na namba yako ya NIDA
– Ingiza namba ya OTP uliyotumwa kwenye namba yako ya simu
– Thibitisha namba yako ya NIDA kwa kujibu maswali marahisi
– Baada ya usajili kukamilika, Piga *150*08# au Fungua App, kisha Ingia.
Utahitaji namba ya NIDA, namba ya simu na kujibu maswali 2 kuthibitisha NIDA yako.
ii. Kusajili kwa Alama ya Kidole
– Kundi la wawakilishi wetu wa Usajili wanapita/kutembea maeneo tofauti tofauti kuwasajili wateja.
– Mteja anaweza kusajiliwa na wawakilishi wetu wa usajili wenye vifaa vya usajili kwa alama ya kidole kwenye vituo mbalimbali vya usajili AU kwenye maduka yote ya Azam (Maduka ya Azam TV na vibanda vyake, maduka ya Azam Ice-cream na maduka ya bidhaa za chakula za Azam).
– Utahitaji Namba ya NIDA na simu yako.

3. Je, nahitaji laini ya Azam kutumia AzamPesa?

AzamPesa haihitaji wala haina laini ya Azam. AzamPesa inatumiwa na mitandao yote, mara baada ya kujisajili unaweza kutumia kwa laini ya mtandao wowote.
– Kwenye mitandao ya Tigo, Airtel na TTCL; AzamPesa inapatikana kwa kupiga *150*08# (USSD) na kwa App.
– Kwenye mitandao ya Vodacom na Halotel – AzamPesa inapatikana kupitia App, mitandao hio ikiruhusu itapatikana kwa kupiga *150*08# (USSD).

4. Ninahitaji nini ili kujisajili?

Kujisajili, utahitaji namba ya simu ya mtandao wowote na namba yako ya NIDA.

5. Kuna Tofauti gani kati ya AzamPesa na Mitandao mingine?

AzamPesa ni tofauti na huduma zingine za kifedha kwasababu zifuatazo:
i. Kujisajili ukiwa na Laini ya Mtandao wowote ule unaoutumia
ii. Kujisajili mwenyewe popote pale kupitia simu janja
iii. Kupata pesa mara mbili; Unapojisajili mwenyewe na Unapofanya muamala wowote wa kwanza.
iv. Kutuma pesa BURE AzamPesa kwenda AzamPesa.
v. Kupata huduma za wakala wa AzamPesa kwenye ofisi zote za Posta nchi nzima
vi. Kufanya miamala yote ya simu kwa kadi ya AzamPesa GUSA bila kutegemea mtandao
vii. Kufanya miamala yote ya simu kwa Unafuu wa hali ya juu kuliko mtandao wowote ule.

6. AzamPesa ina vitu gani ambavyo siwezi kupata kwa Mitandao mingine?

i. OFA ya kurudishiwa pesa. Baada ya kujisajili mwenyewe, kufanya muamala wa kwanza, kulipia vifurushi vya mwezi vya AzamTV, kulipia tiketi za AzamFerry, n.k.
ii. Kufanya miamala kwa gharama nafuu sana
iii. Kadi ya malipo ya AzamPesa GUSA ya kufanya miamala bila mtandao. Zipo za ina tatu:
a) Kadi ya GUSA ya Kawaida
Hii ni aina ya kadi ya Gusa inayotumiwa kufanya miamala ya kawaida ya Azampesa bila kutegemea mtandao pamoja na matumizi mengine ya NCard, kama vile kuingia viwanja vya taifa vya Tanzania. Kadi hii hutumika mijini na vijijini. Kadi hii inawapa uhakika wa kufanya matumizi ya kifedha wateja waliopo vijijini, kwenye maeneo yenye changamoto za mtandao.
b) Kadi ya Shabiki wa AzamFC
Hii ni aina ya kadi ya GUSA inayotumiwa na mashabiki wa AzamFC. Kadi hii ni kadi ya GUSA ya kawaida yenye ongezeko la thamani ya klabu ya AzamFC. Yaani inatumika kufanya miamala na malipo mbalimbali, kukata tiketi za kuangalia mechi za AzamFC, kununua jezi, kupata OFA za bidhaa za klabu, n.k.
c) Kadi za Pesa za Matumizi ya Wanafunzi (Pocket Money Cards)
Hii ni aina ya kadi ya GUSA kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa Bweni na kutwa. Wanafunzi hutumia kadi hii kama kitambulisho na pia kufanya manunuzi mbalimbali wawapo shuleni. Zimeunganishwa na namba ya Azampesa ya wazazi au walezi, hivyo kuruhusu kupata ujumbe wa ripoti ya miamala yote ambayo mwanafunzi ameifanya na kuruhusu wazazi kuongeza salio kwenye kadi ya mwanafunzi bila kufanya mawasiliano.
Jinsi ya Kujisajili
– Tembelea wakala wa GUSA, ukiwa na namba ya NIDA na ya simu.
– Wakala wa GUSA atakusajili na AzamPesa
– Kisha, kuunganisha kadi ya Gusa na namba iliosajiliwa AzamPesa.
– Baada ya usajili kufanikiwa, mteja anaweza kuanza kutumia huduma papo hapo.

Jinsi ya Kutumia:
– Pokea pesa kwenye Azampesa yako
– Tembelea wakala wa GUSA ukiwa na kadi yako ya GUSA.
– Chagua huduma unayohitaji kufanya.
– Weka kadi ya GUSA kwenye kifaa cha Mauzo cha wakala.
– Weka PIN.
Matumizi ya Kadi:
– Tuma pesa.
– Toa pesa.
– Lipa vifurushi vya Azam TV.
– Nunua Muda wa Maongezi

7. Ninaweza kufanya nini na AzamPesa?

Unaweza kufanya miamala mbalimbali na AzamPesa. Kama vile kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua muda wa maongezi, kufanya malipo ya serikali, kulipia huduma za Azam na kufanya miamala ya kibenki.

8. Nawezaje kupata huduma za AzamPesa?

Unaweza kupata huduma za AzamPesa kwa kupiga *150*08# au kupitia App ya AzamPesa kwenye mitandao ya Tigo au Airtel. Kwenye mitandao ya Vodacom na Halotel, kwa sasa inapatikana kupitia App ya AzamPesa tuu, inayopatikana kwenye Google Play Store au iOS App Store.

9. Ninapopiga *150*08#, inasema huduma haipatikani

Ikiwa hauwezi kupata Menyu ya AzamPesa inamaanisha kuwa haujasajiliwa na AzamPesa au unatumia laini ya mtandao wa Vodacom au Halotel. Ikiwa hujasajiliwa, tafadhali angalia hapo juu kwa maelezo ya usajili. Ikiwa una laini ya mtandao wa Vodacom au Halotel, kwa sasa unaweza kupata AzamPesa kupitia App.

10. Wapi naweza kutuma Pesa kwa Azampesa?

Unaweza kutuma kwenda BURE kwenda AzamPesa na kwa gharama nafuu sana kwenda Mitandao mingine au Benki.

11. Nani naweza kumtumia pesa kwa Azampesa?

Unaweza kutuma pesa BURE kwa mtu yeyote aliyesajiliwa na AzamPesa. Pia, unaweza kutuma kwa gharma nafuu kwenda kwa mtu wa mtandao mwingine au Benki.

12. Kikomo cha kutuma pesa ni kipi?

Unaweza kutuma kiasi chochote hadi Tsh milioni 5 kwa mara moja.

13. Wapi naweza kutoa pesa?

Unaweza kutoa pesa kwa mawakala wa AzamPesa walio karibu nawe, kwenye maduka ya AzamTV, maduka ya Azam Ice-cream na maduka ya bidhaa za chakula ya Azam.

14. Jinsi gani naweza kuwasiliana na huduma kwa wateja?

Piga 0800785555 buree bila malipo.

15. Nataka kubadilisha PIN yangu, nifanye nini?

– Piga *150*08#
– Chagua 7 Akaunti Yangu
– Chagua 3 Badilisha PIN
– Ingiza PIN ya zamani
– Ingiza PIN mpya

16. Nimesahau PIN yangu, nifanye nini?

Piga 080078555, Huduma kwa wateja kwa msaada.

17. Nawezaje kuweka pesa kwenye akaunti yangu ya AzamPesa?

Kuna njia tatu za kuweka pesa kwenye akaunti yako ya AzamPesa:
i. Wakala wa AzamPesa:
Tembelea wakala wa AzamPesa karibu na wewe. Wapo:
– Mitaani
– Kwenye ofisi yeyote ya Posta Tanzania nzima na
– Kwenye maduka ya Azam, yaani maduka ya AzamIcecream, AzamTV na AzamFoods.
ii. Pokea pesa
a. Pokea pesa kutoka AzamPesa
– Piga *150*08#
– Chagua 1, Tuma pesa
– Chagua 1, Tuma pesa kwenda AzamPesa
– Weka namba ya simu ikianza na 1 badala ya 0
– Weka kiasi
– PIN

b. Pokea pesa kutoka Mitandao yote Tanzania
– Ingia kwenye menyu ya Mtandao
– Tuma pesa
– Tuma pesa kwenda mitandao mingine
– Tuma kwenda AzamPesa
– Weka namba iliosajiliwa AzamPesa ikianza na 1 badala ya 0. (17XXXXXX61 badala ya 07XXXXXX61)
– Weka kiasi
– PIN

c. Pokea pesa kutoka Benki:
Pokea na Hamisha pesa kutoka Benki nyingi kwenda AzamPesa.
– Ingia kwenye menyu ya Benki
– Hamisha pesa kwenda Mtandao wa simu au Wallet
– Chagua AzamPesa
– Weka namba ya simu ikianzia na 1 badala ya 0.
– Weka kiasi
– PIN
Benki washirika ni kama: CRDB, NMB, NBC, Amana, BOA, ABSA, BanABC, Access Bank, NCBA, DCB, Exim Bank, Finca, Benki ya Maendeleo, PBZ, Stanbic Bank, TCB, Bank of India, Baroda, Canara, China Dasheng, MuCoBa, NCBA, Mwanga Hakika, Habib na ICB.
Kwa msaada wa haraka, piga simu: 0800 785 555 au tutumie ujumbe WhatsApp: 0677 822 222.

18. Je, naweza kununua muda wa maongezi kupitia Azam Pesa?

Ndiyo, unaweza kununua muda wa maongezi wa mtandao wowote, kwa mtu yeyote.
– Piga *150*08#
– Chagua 2, Nunua Muda wa maongezi
– Chagua Mtandao wa Simu
– Weka Namba ya Simu
– Weka Kiasi
– PIN.