
Lipa Hapa na Azampesa
Furahia kufanya malipo ya bili mbalimbali kwa unafuu na haraka zaidi ukitumia Lipa hapa kutoka Azampesa
Kuhusu Lipa Hapa na Azampesa
Azampesa Lipa Hapa ni suluhisho rahisi na la kisasa kwa wafanyabiashara kupokea malipo moja kwa moja kutoka kwa wateja kupitia simu zao! Huduma hii inakupa uwezo wa kupokea pesa kutoka mitandao yote ya simu na benki bila usumbufu wowote
Faida? Ah, ziko nyingi! Unaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yako ya biashara kwenda benki bila gharama, na kutoa pesa kupitia mawakala wa Azampesa au Benki ni nafuu sana, Unahitaji namba ya simu iliyosajiliwa na Azampesa, NIDA na cheti cha TIN ili kupata huduma hii. Malipo yanaweza kufanyika kirahisi kupitia USSD au App ya Azampesa, ukiingiza namba ya biashara ya Azampesa kuthibitisha muamala wako kwa urahisi.
Sasa biashara yako itaruka na Azampesa Lipa Hapa – kupokea malipo imekua rahisi zaidi kuliko unavyofikiria!

Kwa Wafanyabiashara
Huduma za Lipa Hapa
Azampesa Lipa Hapa inakupa huduma bora za malipo kwa biashara yako!
- Pokea malipo kutoka kwa wateja wako bila kutozwa hata senti moja.
- Pokea malipo kutoka kwa wateja wa mitandao yote ya simu na benki.
- Hamisha pesa kwenda benki bila gharama yoyote
- Toa pesa kwa urahisi kupitia mawakala wa Azampesa au benki kama CRDB na NMB
Wafanyabiashara wanaoungwa mkono
Azampesa Lipa Hapa inafanya kazi na biashara za aina zote:
- Maduka ya rejareja
- Migahawa
- Maduka ya Jumla
- Huduma za usafirishaji na zaidi!
Faida kwa Wafanyabiashara
Azampesa inakuwezesha
- Kufuatilia miamala yako kwa urahisi
- Kuboresha usalama wa malipo yako
- Kufikia wateja wengi zaidi kwa kutumia suluhisho za kidijitali
- Kutoa pesa kwa urahisi na kwa bei nafuu
Kwa
Wateja Binafsi
Huduma za Lipa Hapa
Kwa wateja binafsi:
- Ukiwa na Azampesa ukamlipa mtoa huduma kwa Lipa Hapa ya Azampesa utaokoa kiasi kikubwa cha pesa kwa sababu makato yake ni madogo.
- Azampesa Lipa Hapa inafanya malipo kuwa rahisi na haraka.
Jinsi ya kutumia Azampesa Lipa Hapa
Ni rahisi sana kutumia Azampesa Lipa Hapa kwa malipo yako ya kila siku:
1. Kwa USSD:
- Piga *150*08#
- Chagua 5: Lipa Hapa
- Ingiza namba ya biashara, kiasi na thibitisha kwa namba yako ya siri
2. Kwa App ya Azampesa:
- Fungua App ya Azampesa
- Chagua Lipa mtoa huduma
- Ingiza namba ya Biashara na kiasi, kisha thibitisha malipo

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
1. Azampesa Lipa Hapa ni nini?
Azampesa Lipa Hapa ni huduma inayomuwezesha mfanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa au huduma kutoka kwa wateja kupitia simu zao. Wateja wanaweza kulipa kutoka mitandao yote ya simu na hata kupitia benki.
2. Nawezaje kupata Azampesa Lipa Hapa kwa biashara yangu?
Vigezo vya kupata Lipa Hpa ni hivi:
1. Namba ya NIDA
2. TIN ya Biashara
3. Sajili namba utakayotumia iwe na AzamPesa
Kisha tuma kwenda WhatsApp namba 0677099918
3. Jinsi ya kufanya malipo kwa Lipa Hapa ya AzamPesa
Lipia kwa AzamPesa | 1.Piga *150*08# 2.Chagua 5 Lipia bidhaa 3.Chagua 1 Lipa Hapa 4,Chagua 1 Lipa na AzamPesa 5.Andika lipa namba ya AzamPesa 6.Andika kiasi unacholipia 7.Hakiki jina la Lipa namba kisha weka namba ya siri kukamilisha muamala |
Lipia kwa Tigopesa | 1.Piga *150*01# 2.Chagua 5 Lipa kwa Simu 3.Chagua 2 TANQR 4.Andika Lipa namba ya AzamPesa 5.Andika kiasi unacholipia 6.Hakiki jina la lipa namba kisha weka namba ya siri kukamilisha muamala |
Lipia kwa Airtelmoney | 1.Piga *150*60# 2.Chagua 5 lipa bili 3.Chagua 1 lipa kwa simu (mitandao na benki zote) 4.Chagua 5 pay TanQR 5.Andika lipa namba ya AzamPesa 6.Andika kiasi unacholipia 7.Hakiki jina la lipa namba kisha weka namba ya siri kukamilisha muamala |
Lipia kwa Mpesa | 1.Piga *150*00# 2.Chagua 4 lipa kwa Mpesa 3.Chagua 1 lipa kwa simu 4.Chagua 1 Ingiza lipa namba 5.Chagua 3 Azampesa 6.Andika lipa number ya AzamPesa 7.Andika kiasi unacholipia 8.Andika namba ya siri kukamilisha muamala |
Lipia kwa T-Pesa | 1.Piga *150*71# 2.Chagua 6 kwa Lipa namba 3.Chagua 1 TIPS Merchant (All Networks) 4.Andika lipa namba ya AzamPesa 5.Hakiki jina la lipa namba kisha weka namba ya siri kukamilisha muamala |
Lipia kwa Halopesa | 1.Piga *150*08# 2.Chagua 5 Lipia bidhaa 3.Chagua 1 TANQR lipa hapa 4.Andika lipa namba ya AzamPesa 5.Hakiki jina la lipa namba kisha weka namba ya siri kukamilisha muamala |
4. Je, kuna gharama zozote za kuhamisha pesa kutoka akaunti ya Azampesa kwenda benki?
Hakuna gharama yoyote kwako Mfanyabiashara

Tutumie Ujumbe Leo
(WhatsApp)
0677 099 918

Tembelea Ofisi zetu
Makao Makuu
Haile Selassie Rd, Plot 208
Dar es Salaam, Tanzania

Tupigie Bure
Jumatatu – Ijumaa (Saa 24)
0800 785 555

Yote yaliyomo kwenye tovuti hii ni mali ya AzamPesa. Haki zote zimehifadhiwa. Hakimiliki.
Copyright 2025, AzamPesa