AzamPesa ni huduma ya kifedha inayokuwezesha kufanya miamala kwa gharama nafuu zaidi, ukiwa kama mfanyabiashara unahitaji Lipa namba ya Azampesa kwenye biashara yako kukusaidia mambo haya muhimu kwa gharama nafuu zaidi ambayo haiumizi mtaji wako.

  • Gharama Nafuu za Miamala: Kufanya miamala kwa AzamPesa ni nafuu zaidi hivyo humuwezesha mlipaji kuokoa kiasi cha pesa anachoweza kukitumia kwenye matumizi mengine ya msingi.
  • Uhamishaji Pesa: Ni rahisi na nafuu kutoa pesa kwa Wakala wa Azampesa vilevile unaweza kuhamisha pesa kwenda Benki BURE.
  • Usimamizi Bora wa Fedha: Upatikanaji wa taarifa za miamala iliyofanywa muda wowote unapohitaji, na hii inakusaidia kusimamia na kufatilia ukuaji wa biashara yako.

Unaweza kupata Azampesa lipa namba kwa kuwa na nakala hizi:

  • Namba ya simu iliyosajiliwa na AzamPesa.
  • Nida Namba.
  • TIN Certificate.
  • Kitambulisho (Cha Kura,NIDA, Passport au Leseni ya udereva)

Kisha tuma kwenda WhatsApp namba 0677099918.