Huduma Za Azam

Lipia Huduma mbalimbali za Azam kwa AzamPesa.

Kuhusu Huduma

Fanya malipo ya bidhaa mbali mbali za Azam kwa urahisi zaidi kupitia Azampesa.

Kwa kulipia bidhaa za Azam kwa AzamPesa unaweza kupata OFA na PUNGUZO mbali mbali.

 • AzamTv

Ni huduma inayotoa matangazo na maudhui mbalimbali kwa Watanzania, kama vile Habari na Burudani.

Wateja wa AzamTv wanaweza kulipia vifurushi vya ving’amuzi vyao vya AzamTV kiurahisi na kwa haraka kupitia AzamPesa na kupata ofa mbalimbali kama vile kurudishiwa kiasi cha fedha.

 • AzamFerry

Hii ni huduma ya usafirishaji kwa njia ya maji kutoka Daresalaam kwenda Zanzibar.

Okoa muda wa kupanga foleni na kuchelewa kuingia kwenye Boti za Azam kwa kukata tiketi zako mtandaoni na kufanya malipo kwa haraka kupitia AzamPesa

 • SARAFU

Ni duka mtandaoni, mfumo wa biashara wa kidijitali ambao husafirisha bidhaa za madukani/nyumbani kwa maduka madogo na ya kati.

Wateja wa SARAFU wanaweza kulipa Bili zao kirahisi kupitia AzamPesa. Wateja wanatakiwa kwanza kutoa oda zao kupitia SARAFU APP na kuchagua AzamPesa kama njia ya malipo.

Jinsi ya Kutumia

AZAM TV

 1. Piga *150*08#
 2. Chagua 4 Lipia Bili
 3. Chagua 4 Azam Tv
 4. Chagua muda wa kifurushi unachotaka kulipia
 5. Chagua kiwango cha kifurushi unachotaka kulipia
 6. Andika namba ya kadi yako ya king’amuzi
 7. Weka namba ya siri kukamilisha malipo

AU

 1. Fungua App ya AzamPesa
 2. Bofya Huduma za Azam
 3. Bofya AzamTV Vifurushi
 4. Chagua muda wa kifurushi unachotaka kulipia
 5. Chagua kiwango cha kifurushi unachotaka kulipia
 6. Andika namba ya kadi yako ya king’amuzi
 7. Nunua sasa
 8. Hakiki taarifa, kisha Bofya Nunua Kifurushi
 9. Weka namba ya siri kukamilisha malipo

Jinsi ya Kutumia

AZAM FERRY 

 1. Piga *150*08#
 2. Chagua 7 Akaunti yangu
 3. Chagua 6 kuona malipo yaliyosubirishwa
 4. Chagua malipo unayotaka kulipia
 5. Hakiki taarifa
 6. Weka namba ya siri kukamilisha malipo

AU

 1. Fungua App ya AzamPesa
 2. Bofya Akaunti Yangu
 3. Bofya Malipo yaliyosubirishwa
 4. Weka namba ya siri kuona listi
 5. Chagua malipo, kisha Bofya Lipa
 6. Hakiki taarifa, kisha Bofya Fanya Malipo
 7. Weka namba ya siri kukamilisha malipo

Jinsi ya Kutumia

SARAFU

 1. Piga *150*08#
 2. Chagua 7 Akaunti yangu
 3. Chagua 6 kuona malipo yaliyosubirishwa
 4. Chagua malipo unayotaka kulipia
 5. Hakiki taarifa
 6. Weka namba ya siri kukamilisha malipo

AU

 1. Fungua App ya AzamPesa
 2. Bofya Akaunti Yangu
 3. Bofya Malipo yaliyosubirishwa
 4. Weka namba ya siri kuona listi
 5. Chagua malipo, kisha Bofya Lipa
 6. Hakiki taarifa, kisha Bofya Fanya Malipo
 7. Weka namba ya siri kukamilisha

Huduma za Azam Unazoweza Kulipia