AZAMPESA FAQ

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

AzamPesa ni nini?

AzamPesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu inayokuwezesha kufanya miamala kwa gharama nafuu. Kama kutuma na kupokea pesa, kununua muda wa maongezi, kulipa kwa simu kwa mfanyabiashara, kulipa bili kama Luku na maji, kufanya malipo ya serikali, kufanya miamala ya kibenki na kulipia huduma za Azam kama tiketi za Boti, Vifurushi vya ving’amuzi vya AzamTv na zaidi.

Jinsi gani naweza kujisajili na AzamPesa?

Taarifa unazohitaji kusajili AzamPesa:
– Namba ya NIDA
– Namba ya Simu

Njia mbalimbali unazoweza kutumia kujisajili:

i. Kujisajili mwenyewe kwa kuscan vidole

1.Pakua App ya AzamPesa
2. Bofya Usajili Binafsi
3. Chagua Alama za vidole
4. Jaza namba ya simu na namba ya NIDA
5. Weka OTP (namba ya siri uliyotumiwa na AzamPesa)
5. Maelezo ya jinsi ya kuscan vidole kisha chagua mkono wa kuscan
6. Skani vidole
7. Usajili wako umekamilika

 

ii. Kujisajili mwenyewe kwa kuhakiki NIDA
1. Pakua App ya AzamPesa kwenye Google Play Store au iOS App Store
2. Bonyeza USJILI BINAFSI chini ya INGIA
3. Jaza namba yako ya simu na namba yako ya NIDA
4. Ingiza namba ya OTP uliyotumwa kwenye namba yako ya simu
5. Thibitisha namba yako ya NIDA kwa kujibu angalau maswali mawili.
6. Baada ya usajili kukamilika, Piga *150*08# au Fungua App, kisha Ingia.

iii. Kusajili kwa Frilensa wetu
– Kundi la wawakilishi wetu wa Usajili wanapita/kutembea maeneo tofauti tofauti kuwasajili wateja.
– Mteja anaweza kusajiliwa na wawakilishi wetu wa usajili wenye vifaa vya usajili kwa alama ya kidole kwenye vituo mbalimbali vya usajili AU kwenye maduka yote ya Azam (Maduka ya Azam TV na vibanda vyake, maduka ya Azam Ice-cream na maduka ya bidhaa za chakula za Azam).
– Utahitaji Namba ya NIDA na simu yako.

Je, nahitaji laini ya Azam kutumia AzamPesa?

AzamPesa haihitaji wala haina laini ya Azam. AzamPesa inatumiwa na mitandao yote, mara baada ya kujisajili unaweza kutumia kwa laini ya mtandao wowote.

Nahitaji nini ili kujisajili?

Kujisajili, utahitaji namba ya simu ya mtandao wowote na namba yako ya NIDA.

Kuna Tofauti gani kati ya AzamPesa na Mitandao mingine?

AzamPesa ni tofauti na huduma zingine za kifedha kwasababu zifuatazo:
i. Kujisajili ukiwa na Laini ya Mtandao wowote ule unaoutumia
ii. Kujisajili mwenyewe popote pale kupitia simu janja
iii. Kutuma pesa BURE AzamPesa kwenda AzamPesa.

Ninaweza kufanya nini na AzamPesa?

Unaweza kufanya miamala mbalimbali na AzamPesa. Kama vile kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua muda wa maongezi, kufanya malipo ya serikali, kulipia huduma za Azam na kufanya miamala ya kibenki.

Nawezaje kupata huduma za AzamPesa?

Unaweza kupata huduma za AzamPesa kwa kupiga *150*08# au kupitia App ya AzamPesa kwenye mitandao ya Tigo au Airtel. Kwenye mitandao ya Vodacom na Halotel, kwa sasa inapatikana kupitia App ya AzamPesa tuu, inayopatikana kwenye Google Play Store au iOS App Store.

Ninapopiga *150*08#, inasema huduma haipatikani

Ikiwa hauwezi kupata Menyu ya AzamPesa inamaanisha kuwa haujasajiliwa na AzamPesa au unatumia laini ya mtandao wa Vodacom au Halotel. Ikiwa hujasajiliwa, tafadhali angalia hapo juu kwa maelezo ya usajili. Ikiwa una laini ya mtandao wa Vodacom au Halotel, kwa sasa unaweza kupata AzamPesa kupitia App.

Wapi naweza kutuma Pesa kwa Azampesa?

Unaweza kutuma kwenda BURE kwenda AzamPesa na kwa gharama nafuu sana kwenda Mitandao mingine au Benki.

Nani naweza kumtumia pesa kwa Azampesa?

Unaweza kutuma pesa kwa mitandao mingine na benki kwa gharama nafuu. Hata hivyo, unaweza kumshauri mteja unayetaka kumtumia pesa ajisajili na AzamPesa, ili muweze kufurahia kutumiana pesa BURE kutoka AzamPesa kwenda AzamPesa.

Kikomo cha kutuma pesa ni kipi?

Unaweza kutuma kiasi chochote hadi Tsh milioni 5.

Wapi naweza kutoa pesa?

Unaweza kutoa pesa kwa mawakala wa AzamPesa walio karibu nawe, kwenye maduka ya AzamTV, maduka ya Azam Ice-cream na maduka ya bidhaa za chakula ya Azam.

Jinsi gani naweza kuwasiliana na huduma kwa wateja?

Piga 0800785555 bure bila malipo.

Nataka kubadilisha PIN yangu, nifanye nini?

– Piga *150*08#
– Chagua 7 Akaunti Yangu
– Chagua 3 Badilisha PIN
– Ingiza PIN ya zamani
– Ingiza PIN mpya

Nimesahau PIN yangu, nifanye nini?

Piga 080078555, Huduma kwa wateja kwa msaada.

Nawezaje kuweka pesa kwenye akaunti yangu ya AzamPesa?

i. Wakala wa AzamPesa:
Tembelea wakala wa AzamPesa aliye karibu nawe ili kuweka pesa kwenye akaunti yako. Wakala wanapatikana:

  • Katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania

  • Katika ofisi zote za Posta Tanzania

  • Katika maduka ya Azam (Maduka ya Ice-cream ya Azam, maduka ya AzamTV, na maduka ya bidhaa za chakula za Azam)


ii. Pokea Pesa:

a) Kupokea kutoka kwenye pochi ya AzamPesa:

  • Piga 15008#

  • Chagua 1, Tuma Pesa

  • Chagua 1, Tuma Pesa kwenda AzamPesa

  • Weka namba ya AzamPesa ya mpokeaji

  • Weka kiasi

  • Weka PIN

b) Kupokea kutoka mitandao mingine ya simu:

  • Piga menyu ya huduma ya kutuma pesa ya mtandao husika

  • Chagua “Tuma Pesa”

  • Chagua “Tuma Pesa kwenda Mitandao Mingine”

  • Chagua kutuma kwenda AzamPesa

  • Weka namba ya simu iliyosajiliwa na AzamPesa (anza na 1 badala ya 0)

  • Weka kiasi

  • Weka PIN

c) Kupokea kutoka Benki:
Unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka benki yoyote kwenda AzamPesa:

  • Ingia kwenye menyu ya huduma za benki

  • Chagua “Tuma Pesa kwenda Pochi ya Simu” au “Wallet”

  • Chagua AzamPesa

  • Weka namba ya AzamPesa iliyosajiliwa (anza na 1 badala ya 0)

  • Weka kiasi

  • Weka PIN

Benki washirika ni pamoja na:
CRDB, NMB, NBC, Amana, BOA, ABSA, BancABC, Access Bank, NCBA, DCB, Exim Bank, Finca, Maendeleo Bank, PBZ, Stanbic Bank, TCB, Bank of India, Bank of Baroda, Canara, China Dasheng, MuCoBa, NCBA, Mwanga Hakika, Habib, na ICB.

Je, naweza kununua muda wa maongezi kupitia Azam Pesa?

Ndiyo, 

  • Unaweza kununua muda wa maongezi wa mtandao wowote wa simu ukitumia AzamPesa.
  • Unaweza kununua muda wa maongezi kwa mtu mwingine wa mtandao wowote kupitia AzamPesa pia.