Huduma Za Benki

Huduma za Kibenki na AzamPesa

Kuhusu Huduma

AzamPesa inakuwezesha kufanya huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi. 

Unaweza kuhamisha Pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Benki kwenda AzamPesa na kuhamisha Pesa Kutoka AzamPesa kwenda kwenye akaunti ya benki.

Mteja anatakiwa kuunganisha namba yake ya simu na akaunti yake ya benki kuweza kufanya huduma hizi.

Kwa maelezo zaidi tembelea tawi lolote la benki unayotumia lililo karibu nawe.

Jinsi Inavyofanya Kazi

  1. Piga *150*08#
  2. Chagua 6 Huduma za Benki
  3. Chagua 1 AzamPesa kwenda Benki AU 2 Benki kwenda AzamPesa
  4. Chagua Benki na ufuate maelekezo

AU

  1. Fungua App ya AzamPesa
  2. Bofya Hamisha kwenda Benki
  3. Weka Akaunti Namba
  4. Weka Kiasi
  5. Hakiki taarifa zako, kisha Bofya Thibitisha Tuma
  6. Weka PIN yako ya AzamPesa, kisha Thibitisha

Baadhi ya Benki washirika