AzamPesa ni Nini?

AzamPesa ni huduma ya pesa kwa njia ya simu inayokuwezesha kufanya kufanya miamala kwa gharama nafuu. Hii inajumuisha kutuma na kupokea pesa, kununua vocha za muda wa maongezi, malipo ya wafanyabiashara, kulipa bili kama vile umeme na maji, malipo ya serikali, kufanya uhamisho wa pesa kwenye benki, na kulipia huduma za Azam kama tiketi za boti za Azam, vifurushi vya AzamTV, bili za Sarafu, na mengine mengi.

 

Unaweza kujisajili AzamPesa ukiwa na laini yoyote ya simu. Ndio, haijalishi uko kwenye mtandao gani wa simu, AzamPesa inafanya kazi kwa kila mtu. Hii inamaanisha urahisi zaidi katika kufanya miamala kwa njia ya simu.

Nini Kinachofanya AzamPesa Kuwa Tofauti?

Miamala Bure (AzamPesa kwenda AzamPesa):
Ukimtumia pesa mtu mwingine ambaye pia anatumia AzamPesa, hutalazimika kuwa na wasiwasi kuhusu ada, ni bure. Hakuna ada za miamala. Fikiria ni kiasi gani unaweza kuokoa ikiwa unamtumia pesa rafiki au familia mara kwa mara.

Ada za Chini kwenye Miamala Mingine:
AzamPesa ina gharama za makato za chini zaidi sokoni. Ukitumia AzamPesa unaokoa pesa zaidi kila unapohamisha pesa zako kwenda mtandao mwingine. Unaweza kuokoa hadi 20% ikilinganishwa na majukwaa mengine.

Sisi ni Watanzania Halisi:
AzamPesa ni kampuni iliyoundwa na kampuni ya Kitanzania ambayo inaelewa mahitaji ya watu wanaowahudumia. Tunajua ni muhimu kiasi gani kwa Watanzania kupata suluhisho la kifedha linaloaminika, nafuu, na rahisi. Kuunga mkono AzamPesa ni kuunga mkono watanzania wenzio.  

Hatua za Kujisajili na AzamPesa:

Kujisajili Mwenyewe:

  1. Pakua App ya AzamPesa.
  2. Bonyeza “Jisajili Mwenyewe.”
  3. Weka namba yako ya simu na namba ya NIDA.
  4. Weka namba ya OTP (msimbo wa siri wa wakati mmoja) uliotumwa na AzamPesa.
  5. Jibu maswali mawili kutoka NIDA ili kuthibitisha utambulisho wako.
  6. Usajili wako utakamilika!

 

Unaweza pia kujiandikisha na wawakilishi wetu wa usajili wa AzamPesa (Frilensa) ambao wanapatikana katika eneo lako na kwenye maduka yoyote ya Azam, kama AzamTV, Azam Ice Cream, Bidhaa za Chakula za Azam, na Azam Marine.

Kwanini Utumie AzamPesa?

Sasa, unaweza kuwa unafikiria: Kwa nini nibadilike kwenda AzamPesa wakati kuna sehemu nyingine niliyoizoea? Swali zuri. 

  • Ni Nafuu: Ada za chini na uhamisho wa bure wa AzamPesa kwenda AzamPesa zinamaanisha unaendelea kuhifadhi pesa zako zaidi. Nani hapendi hivyo?
  • AzamPesa inakua haraka, na tunazidi kuongeza vipengele vipya ili kuifanya kuwa bora zaidi. 

Kama bado hujajiunga na AzamPesa, unasubiri nini? Pakua app na jisajili, Tumia AzamPesa, na uanze kufurahia maisha bila makato mzigo.

Kwa maswali zaidi, tafadhali tupigie 0800 785 555 BURE tutakusaidia.

#JiokoeNaAzamPesa

Recent Posts

Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Mitandao Mingine Kuja AzamPesa

Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Mitandao Mingine Kuja AzamPesa

AzamPesa pia inakuwezesha kupokea pesa kutoka mitandao mingine kwa urahisi. Hivi ndivyo unavyoweza kufanya: Kutoka M-Pesa Kwenda AzamPesa Piga *150*00#. Chagua Kutuma Pesa. Chagua Kutuma Kwa Mitandao Mingine. Chagua chaguo la 5 kwa AzamPesa. Ingiza namba ya AzamPesa...

Faida za Kutumia AzamPesa: Huduma Bora na Unafuu Kwa Mahitaji Yako

Faida za Kutumia AzamPesa: Huduma Bora na Unafuu Kwa Mahitaji Yako

AzamPesa inaleta mapinduzi katika ulimwengu wa huduma za kifedha kwa kutoa unafuu wa gharama, usalama wa hali ya juu, na urahisi wa kufanya miamala. Hizi hapa ni faida na huduma unazoweza kufurahia unapojisajili na kutumia AzamPesa.1. Faida za Kutumia AzamPesa Miamala...

Jinsi ya Kujisajili AzamPesa kwa Urahisi

Jinsi ya Kujisajili AzamPesa kwa Urahisi

Unataka kujisajili AzamPesa ili uanze kufurahia gharama nafuu za makato? Kujisajili AzamPesa ni rahisi mno.  Ili uweze kujisajili, hatua ya kwanza ni kupakua app ya AzamPesa ambayo inapatikana playstore na appstore. HATUA ZA KUJISAJILI KWA WATUMIAJI WA ANDROID 1....