AzamPesa ni Nini?
AzamPesa ni huduma ya pesa kwa njia ya simu inayokuwezesha kufanya kufanya miamala kwa gharama nafuu. Hii inajumuisha kutuma na kupokea pesa, kununua vocha za muda wa maongezi, malipo ya wafanyabiashara, kulipa bili kama vile umeme na maji, malipo ya serikali, kufanya uhamisho wa pesa kwenye benki, na kulipia huduma za Azam kama tiketi za boti za Azam, vifurushi vya AzamTV, bili za Sarafu, na mengine mengi.
Unaweza kujisajili AzamPesa ukiwa na laini yoyote ya simu. Ndio, haijalishi uko kwenye mtandao gani wa simu, AzamPesa inafanya kazi kwa kila mtu. Hii inamaanisha urahisi zaidi katika kufanya miamala kwa njia ya simu.

Nini Kinachofanya AzamPesa Kuwa Tofauti?
Miamala Bure (AzamPesa kwenda AzamPesa):
Ukimtumia pesa mtu mwingine ambaye pia anatumia AzamPesa, hutalazimika kuwa na wasiwasi kuhusu ada, ni bure. Hakuna ada za miamala. Fikiria ni kiasi gani unaweza kuokoa ikiwa unamtumia pesa rafiki au familia mara kwa mara.
Ada za Chini kwenye Miamala Mingine:
AzamPesa ina gharama za makato za chini zaidi sokoni. Ukitumia AzamPesa unaokoa pesa zaidi kila unapohamisha pesa zako kwenda mtandao mwingine. Unaweza kuokoa hadi 20% ikilinganishwa na majukwaa mengine.
Sisi ni Watanzania Halisi:
AzamPesa ni kampuni iliyoundwa na kampuni ya Kitanzania ambayo inaelewa mahitaji ya watu wanaowahudumia. Tunajua ni muhimu kiasi gani kwa Watanzania kupata suluhisho la kifedha linaloaminika, nafuu, na rahisi. Kuunga mkono AzamPesa ni kuunga mkono watanzania wenzio.
Hatua za Kujisajili na AzamPesa:
Kujisajili Mwenyewe:
- Pakua App ya AzamPesa.
- Bonyeza “Jisajili Mwenyewe.”
- Weka namba yako ya simu na namba ya NIDA.
- Weka namba ya OTP (msimbo wa siri wa wakati mmoja) uliotumwa na AzamPesa.
- Jibu maswali mawili kutoka NIDA ili kuthibitisha utambulisho wako.
- Usajili wako utakamilika!

Unaweza pia kujiandikisha na wawakilishi wetu wa usajili wa AzamPesa (Frilensa) ambao wanapatikana katika eneo lako na kwenye maduka yoyote ya Azam, kama AzamTV, Azam Ice Cream, Bidhaa za Chakula za Azam, na Azam Marine.
Kwanini Utumie AzamPesa?
Recent Posts
JE WAJUA!
Unaweza kuokoa pesa ukitumia Azampesa Ikiwa wewe ni mtumiaji wa kawaida na unafanya miamala ya kutuma pesa na unatuma kati ya shilingi 10,000 hadi 20,000 kwa siku, basi unajua makato yake kila unapofanya miamala ni makubwa. Kwa mfano, ukiweza kutuma pesa mara mbili...
Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Mitandao Mingine Kuja AzamPesa
Faida za Kutumia AzamPesa: Huduma Bora na Unafuu Kwa Mahitaji Yako
AzamPesa inaleta mapinduzi katika ulimwengu wa huduma za kifedha kwa kutoa unafuu wa gharama, usalama wa hali ya juu, na urahisi wa kufanya miamala. Hizi hapa ni faida na huduma unazoweza kufurahia unapojisajili na kutumia AzamPesa.1. Faida za Kutumia AzamPesa Miamala...
Jinsi ya Kutuma Pesa kwa Gharama Nafuu Kutoka AzamPesa Kwenda Mitandao Mingine
Urahisi wa kutuma pesa kupitia mitandao mbalimbali ya simu ni muhimu sana. AzamPesa inafanya mchakato huu kuwa rahisi, salama, na haraka. Jinsi ya Kutuma Pesa Kutoka AzamPesa Kwenda TigoPesa / EzyPesa Kwa kutumia App ya AzamPesa: Fungua App yako ya AzamPesa. Chagua...
Jinsi ya Kujisajili AzamPesa kwa Urahisi

Yote yaliyomo kwenye tovuti hii ni mali ya AzamPesa. Haki zote zimehifadhiwa. Hakimiliki.
Copyright 2025, AzamPesa