AzamPesa inaleta mapinduzi katika ulimwengu wa huduma za kifedha kwa kutoa unafuu wa gharama, usalama wa hali ya juu, na urahisi wa kufanya miamala. Hizi hapa ni faida na huduma unazoweza kufurahia unapojisajili na kutumia AzamPesa.
1. Faida za Kutumia AzamPesa
- Miamala ya Unafuu: AzamPesa inakupa nafasi ya kufanya miamala kwa gharama ndogo, ukitunza pesa zako bila makato makubwa.
- Huduma bila Mtandao: Kupitia kadi ya GUSA, unaweza kufanya miamala bila mtandao popote ulipo.
- Usalama wa Pesa: Akaunti yako ya AzamPesa inalindwa na teknolojia za hali ya juu, kuhakikisha pesa zako ziko salama.
- Kadi ya GUSA: Kadi hii inakuruhusu kutumia AzamPesa kununua tiketi za mechi mbali mabli za mpira wa miguu.
- OFA za Huduma za Azam: Unapata punguzo na zawadi unapotumia AzamPesa kulipia huduma mbali mbali za Azam.
2. Ofa Zinazopatikana kwa Watumiaji wa AzamPesa
- Kutuma pesa BURE kutoka AzamPesa kwenda AzamPesa.
- Kupata unafuu wa miamala.
- Kurudishiwa pesa unaponunua vifurushi vya AzamTV au tiketi za boti za AzamMarine.
- Kurudishiwa asilimia 1 ya thamani ya manunuzi yako unapofanya manunuzi ya SARAFU.
- Kupata kadi ya GUSA ya kufanya miamala bila mtandao.
3. Njia za Kufanya Miamala na AzamPesa
- Kupiga Code: Tumie *150*08# kwenye simu yoyote kufanya miamala.
- Kupitia App ya AzamPesa: Pakua app kwenye Google Playstore au App Store kwa urahisi zaidi.
- Kadi ya GUSA: Tumia kufanya malipo kupitia POS au mifumo ya NCARD.
4. Mipaka ya Miamala
- Unaweza kutuma pesa hadi milioni 5 kwa siku.
- Unaweza kupokea pesa hadi milioni 10 kwa siku.
5. Njia za Kulinda Akaunti Yako
- Kujiandikisha kwa kutumia OTP (namba ya siri) inayotumwa na AzamPesa.
- Kulinda miamala kwa PIN binafsi na swali la siri.
- Usalama wa kipekee wa App ya AzamPesa, ikiwa ni pamoja na kukosa uwezo wa kuchukua picha za skrini kwa Android.
- OTP inahitajika unapotumia App kwenye simu mpya.
6. Jinsi ya Kuwasiliana na Huduma kwa Wateja
Tunakuhakikishia msaada wa haraka kupitia njia zifuatazo:
- Simu: Piga bure 0800785555.
- WhatsApp: Tuma ujumbe kwa +255 677 822 222.
- Barua Pepe: Tuma barua pepe kwenda info@azampesa.co.tz.
Kwa kutumia AzamPesa, unapata huduma bora, salama, na nafuu zinazokidhi mahitaji yako ya kifedha. Jiunge leo na ufurahie urahisi wa kufanya miamala popote ulipo!