Kuwa Wakala Ujipatie Kamisheni Nono

Wakala wa Azampesa ni Mshirika rasmi wa AzamPesa anayetoa huduma za kifedha kama kuweka na kutoa pesa, kuuza muda wa maongezi na vifurushi vya AzamTv kwa wateja. Wakala pia husaidia katika masuala ya huduma kwa wateja, huku wakipata kamisheni kwa kila muamala unaofanyika kupitia huduma zao.

Faida za kuwa wakala

  • Kamisheni kubwa zaidi kulinganisha na mitandao mengine
  • Unaweza kumwekea mteja pesa
  • Mteja anaweza kutoa pesa
  • Kuuza muda wa maongezi na vifurushi vya azamtv kujipatia kamisheni
  • Wakala anaweza kutumia mtandao wowote kuunganisha uwakala wa azampesa

Vigezo vya Kuwa Wakala Wa Azampesa

Ili kuwa wakala wa Azampesa tuma nakala hizi kwenda WhatsApp namba 0677 099918

 

  • Namba ya NIDA
  • TIN ya Biashara
  • ⁠Sajili namba utakayotumia kuwa Wakala wa AzamPesa

 

Kwa msaada zaidi tupigie simu BURE 0800 785 555

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)

1. Ni huduma zipi ambazo wakala wa AzamPesa anaweza kuzitoa?

Kumuwekea mteja salio, kumsaidia mteja kutoa pesa, kuunga vifurushi vya AzamTv na kuuza muda wa maongezi

2. Nawezaje kumuwekea mteja hela?

1.Fungua App ya AzamPesa Wakala
2.Chagua Weka Pesa
3.Ingiza namba ya mpokeaji
4.Ingiza kiasi unachotaka kutuma
5.Bofya Endelea
6.Hakiki taarifa kisha tuma pesa

3. Jinsi wakala anaweza kuuza muda wa maongezi.

KWA KUTUMIA APP
1.Fungua App ya AzamPesa Wakala
2.Chagua Fanya Mauzo
3.Chagua Uza Muda wa Maongezi
4.Chagua Mtandao wa simu
5.Ingiza namba ya simu
6.Ingiza kiasi cha kutuma
8.Hakiki taarifa kisha bofya Uza Muda wa Maongezi

Wakala anaweza kuuza muda wa maongezi kuanzia Tsh 500/= na anapata bonus ya asilimia mbili ya muda wa maongezi atakayouza.

4. Wapi naweza kupata floti?

1. Wakala mkuu wa Azampesa
2. Ofisi za Posta Tanzania
3. Matawi ya Benki ya NMB na CRDB

Kwa maelezo zaidi tuwasiliane BURE kupitia namba 0800 785 555.

Tutumie Ujumbe Leo

(WhatsApp)
0677 099 918

Tembelea Ofisi zetu

Makao Makuu
Haile Selassie Rd, Plot 208
Dar es Salaam, Tanzania

Tupigie Bure

Jumatatu – Ijumaa (Saa 24)
0800 785 555

Copyright 2025, AzamPesa